loader image

News

Read our latest news, corporate updates, and key developments.

ZIC YAFUTARISHA WADAU WA BIMA ZANZIBAR KUIMARISHA USHIRIKIANO

Shirika la Bima la Zanzibar limeandaa hafla ya futari (Iftar) kwa wadau wake mbalimbali katika Hoteli ya Verde iliyopo Mtoni Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya shirika hilo na taasisi mbalimbali zinazoshirikiana nalo katika utoaji wa huduma za bima.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Juma Malik Akil, ambaye alipongeza juhudi za Shirika la Bima la Zanzibar katika kuimarisha sekta ya bima
na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Zanzibar kupitia huduma zake.
Katika hotuba yake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bw. Ali Mzee Ali alieleza kuwa hafla hiyo ni sehemu ya utamaduni wa shirika wa kukutana na wadau wake katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kujadiliana mafanikio yaliyopatikana pamoja na kuimarisha mikakati ya baadaye ya kukuza sekta ya bima Zanzibar.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Bima la Zanzibar, Bw. Jape Ussi Khamis, alisema shirika linaendelea kubuni na kuboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji ya wananchi na taasisi mbalimbali, huku likiimarisha ushirikiano na sekta ya benki na wadau wengine muhimu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wakuu wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi, madalali na mawakala wa bima, pamoja na wawakilishi wa mabenki yanayoshirikiana na Shirika la Bima la Zanzibar katika
utoaji wa huduma za bima.
Shirika la Bima la Zanzibar linaendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za bima nchini na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa Zanzibar kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha.

For all your Insurance requirement please contact Zanzibar Insurance Head office in Zanzibar, Zonal offices and our intermediaries through out the country.

Contacts

Our Head Office

Bima House No: 1 Mpirani-Street
Mlandege Road P.O.Box 432
71102 Urban West, Zanzibar

Scroll to Top